Ni
siku chache tu zimepita toka Paul Okoye wa kundi la P-Square afanye
harusi ya kimila na mke wake Anita Isama huko Nigeria, lakini baada ya
wote wawili (Peter & Paul) kukamilisha majukumu ya ndoa zao, kuna
habari
ambazo zimesambaa wiki hii kuwa umeibuka ugomvi baina ya mapacha hao wa kundi la P-Square ambao inasemekana sasa hawaelewani vizuri.
ambazo zimesambaa wiki hii kuwa umeibuka ugomvi baina ya mapacha hao wa kundi la P-Square ambao inasemekana sasa hawaelewani vizuri.
Kama
unakumbuka Jude hakuhudhuria harusi ya Peter na Lola mwaka jana, lakini
alihudhuria ya Paul na Anita mwaka huu kitu kinachowafanya watu waamini
kuwa kuna tatizo kubwa baina yao.
Chanzo
hicho kimesema inadaiwa kuwa ugomvi huo unaomhusu Lola umesababisha
Peter na Paul kugombana wakati wako kwenye rehearsle Jumatano wiki hii,
mpaka walipoachanishwa na dancers wao.
Kaka mkubwa wa P-Square Jude alitweet kitu ambacho kinaaminika kuwa kinahusiana na ugomvi wao.
“After
over 10 years of hard work, it’s over. (I) Am done.” ikiaminika kuwa
alimaanisha amejiondoa kuli-manage kundi hilo japo kuwa yeye mwenyewe
hakufafanua alichomaanisha katika maneno hayo machache.
After over 10yrs of hard work, it's over. Am done.
— IG: @Judeengees (@judeengees) April 18, 2014
Jude
ndiye amekuwa akiwa-manage kwa miaka yote na kuproduce hits zao paomoja
na kudirect idadi kubwa ya video zao zilizofanya vizuri.
Lakini
kuna baadhi ya watu nchini Nigeria wamedai kubwa kuna uwezekano kuwa
ugomvi ‘hewa’ unaoendelea na kuripotiwa katika vyombo vya habari ukawa
ni ‘hype’ ya kuandaa ‘kiki’ ya album yao mpya.
0 comments:
Post a Comment