Meli ya China inayofanya kazi ya kutafuta
ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia iliyopotea maeneo ya Kusini mwa
Bahari ya Hindi imepata ishara inayodaiwa kutoka kwenye ndege hiyo,
vimesema vyombo vya habari vya China.Vilisema
ishara hiyo ilikuwa na marudio ya frikwensi ya 37.5kHz kwa sekunde
ambayo ni sawa na ile iliyozalishwa na kinasa sauti cha ndege.
Hata hivyo hakuna ushahidi hadi sasa kama inahusika moja kwa moja na ndege hiyo H370.
Dazeni ya meli na ndege zimeungana
kutafuta ndege hiyo, huku operesheni hiyo ikiwa katika kuingia kwa kina
katika awamu nyingine ya kutafuta kabla ya betri ya kurekodi data
kufifia.
0 comments:
Post a Comment