Blogger Tricks

LINKS

Friday, 21 February 2014

MASHOGA NA WASAGAJI WAAANDAMANA HAPA SFRIKA KUSINI KUELEKEA MAHAKAMA KUU,ANGALIA PICHA

Chama cha mashoga na wasagaji hapa Afrika Kusini (CAL)
jana kiliandamana kwa mara nyingine kuelekea mahakama kuu kupinga hatua ya idara ya uhamiaji kumkamata daktari raia wa Uganda ambaye ni shoga.

Daktari huyo ambaye anafahamika kama Paul Nsubuga Semugoma  na ambaye ni shoga alikamatwa siku ya jumapili akitokea nchi ya Zimbabwe ambako alikwenda kwenye mikutano yake ya kikazi.

Daktari huyo ambaye alikuwa anaishi hapa  toka mwaka 2012 yalimkuta masaibu hayo katika uwanja wa ndege wa kimataifa uliopo hapa Johannesburg baada ya  mawasiliano ya idara ya uhamiaji kutokuwa mazuri na hivyo kufunguliwa kesi ya kuingia nchi ya Afrka Kusini bila ya kuwa vibali.Na hivyo idara hiyo kuamua kutaka mrudisha kwao Uganda.

Hali hiyo ikapelekea vyama vya mashoga na wasagaji hapa kupeleka kesi mahakama kuu ya kutaka daktari huyo aachiwe na idara hiyo kwani kitendo cha kurudishwa Uganda maisha yake yatakuwa hatarini kutokana na sheria walioiweka Uganda dhidi ya mashoga na wasagaji.

Uganda siku za hivi karibuni imetengeneza vichwa vingi vya habari duniani baada ya kupitisha sheria ya kutovaa nguo fupi kwa wanawake huku wakikaribia kupitisha sheria kwa mashoga na wasagaji

0 comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

About

 
Tricks and Tips