Siku ya jumamosi chama cha siasa cha EFF hapa Afrika Kusini kiliiweka ilani yake ya uchaguzi wazi kwa wanachama na wananchi wote wa hapa Afrika Kusini kwa ujumla kuelekea uchaguzi mkuu
wa mwaka huu
Katika ilani hiyo ya uchaguzi kiongozi wa chama hicho Julius Malema aliwakosha wanachama wake elfu hamsini waliofika katika viwanja hivyo vilivyopo nje ya jiji la Johannesburg kwa hotuba ya ilani yake hiyo ya uchaguzi.
Amesema kuwa hata kama atakufa angependa siku moja wananchi wa Afrka Kusini wakombolewe kupitia chama chake hicho.Huku akiwaambia kuwa chama chake kimepania kuwakomboa wananchi wa Afrika Kusini toka utawala wa wenye nacho unaoongozwa na chama cha ANC.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na wananchi toka miji tofauti hapa Afrika Kusini ulikuwa wa kipekee na wa aina yake kutokana na kuwa wa kuvutia kwa kila mtu aliyekuwepo siku hiyo.
.
Wednesday, 26 February 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment