Makocha wa zamani pamoja na wachezaji wa wa timu ya taifa ya Afrika Kusini wamekuja na mpango kabambe unaoitwa okoa Afrika Kusini.Mpango huo unakuja baada ya timu ya taifa ya hapa kufanya vibaya katika michuano yake yote walioindalia kuanzia kombe la dunia la mwaka 2010,kombe la mataifa ya Afrika ya mwaka 2012,kombe la mataifa ya Afrka mwaka 2013 pamoja na kombe la mataifa ya Afrka kwa wachezaji wa ndani 2014.
Hali hyo ikaleta mtafaruku wa wapi timu ya taifa ya mpira wa miguu inakoelekea na hivyo kupelekea waziri wa michezo wa hapa mh.Fikile Mbalula kuwaita wachezaji hao katika kugha ya kigeni kuwa ni BUNCH OF LOOSERS.
Baada ya matokeo hayo yote mabaya ya timu kwa udhamini wa benk ya NEDBANK sasa imechukua makocha wa zamani kama lashe Mashaba aliyekuwa kocha wa vijana chini ya umri wa miaka 23.Owen Dagama aliyekuwa kocha wa platinum stars pamoja na mchezaji wa zamani wa timu hiyo na pia ni kocha msaidizi wa Kaiza Chief.Makocha hao sasa wameenda kila jimbo la hapa Afrka Kusini na kutafuta vipaji ambavyo viatakuja kuwa mwakilishi wa taifa hili hapo baadae.Angalia picha hizo tofauti katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Ligi kuu ya Afrika Kusini na kuwatambulisha baadhi ya wachezaji hao hapo juzi.
Sunday, 2 February 2014
BAADA YA TIMU YA SOKA YA AFRIKA KUSINI KUVURUNDA KATIKA MICHUANO YOTE WALIOINDAA,JE UNAUJUA MPANGO WALIOKUJA NAO MAKOCHA WA HAPA KULISAIDIA TAIFA HILO?
Labels:
SPORTS
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment