Blogger Tricks

LINKS

Wednesday, 19 February 2014

UNAUJUA MKUTANO ULIOIPITISHA DSM KUWA MWANACHAMA WA MIJI MIKUBWA DUNIANI? JE UNAWAJUA NI VIONGOZI GANI WALIOIPITISHA DSM? ANGALIA PICHA HAPO CHINI

C40 ndio mkutano ulioipitisha DSM kuwa mwanachama wa miji mikubwa kabisa duniani,mkutano huu ulifanyika hapa Johannesburg hivi karibuni na kuyapitisha maazimio hayo.
                                  Meya wa DSM Dr Didas Masaburi akizungu8mza katika mkutano huo

Kabla ya Dsm
kuwa mwanachama wa umoja huo wa miji mikubwa duniani hapo kabla kulikuwa na miji minne tu iliyoingia katika umoja huo kwa vigezo ambavyo c40 wanavihitaji,na miji hiyo ni Johannesburg toka hapa Afrika Kusini,Abuja toka Nigeria,Cairo toka Misri pamoja Adiss Ababa toka Ethiopia.
                                           mwenyekiti wa mstaafu wa c40 Michael Bloomberg

Kwa maana hiyo mpaka sasa miji toka Afrika imeongezeka na kuwa saba baada Dsm toka Tanzania,Nairobi toka Kenya  pamoja na Cape Town toka hapa Afrika Kusini.
                                                 Mameya waliokuwa katika mkutano huo

Mameya toka miji mikubwa kabisa duniani ndio waliopitisha maazimio hayo hapa Johannesburg na hivyo kuifanya Dsm kuipita miji mikubwa toka bara la Afrika na mengineyo sababu wanachama wa c40 ni miji 39 mikubwa toka dunia nzima.


  

Mwenyeji wa mkutano huo meya toka Johannesburg Parks Tau

Na hizo picha hapo chini ni za mameya hao toka duniani huku meya wa DSM Dr Didas Masaburi akiwepo 
miongoni mwao katika mkutano huo wa c40.


0 comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

About

 
Tricks and Tips