Blogger Tricks

LINKS

Friday, 21 February 2014

JE,UNAMJUA KIJANA MWENYE USHAWISHI TOKA KATIKA BARA LA AFRIKA,AMBAYE AMEINGIA KATIKA ORODHA YA WATU 100 BORA WENYE USHAWISHI MKUBWA DUNIANI?

Julius Malema ndiye kijana mwenye ushawishi kabisa duniani kwa sasa,alikuwa rais wa
vijana wa chama tawala cha Afrika Kusini cha ANC kabla ya kufukuzwa kwake katika chama hicho na uongozi wa ANC  mwaka 2011.

Kama hujui sifa za jamaa huyu ni ushawishi aliokuwa nao kwa jamii kubwa ya hapa Afrika Kusini.Yeye ndiye aliyeleta kampeni enzi za mgogoro wa chama hicho wa mwaka 2006 kati ya rais wa kipindi hicho Thabo Mbeki na waziri wake wa mambo ya nje ambaye kwa sasa ndiye rais wa hapa Jackob Zuma kwa kumpigia kampeni Jackob Zuma katika uchaguzi wa ndani wa chama  kati ya mahasimu hao wawili hivyo Zuma kuibuka mshindi wa mwenyekiti wa chama hicho tawala.

Kwa sasa baada ya kusimamishwa toka chama cha ANC kwa miaka mitano ameamua kuja na chama chake mwenyewe kiitwacho EFF yaani ECONOMICAL FREEDOM FIGHTER.

Baada ya kuunda chama chake yani ni kama ameondoka na vijana wengi kwani ushawishi wake umemfanya kuwa na wanachama wengi kwa muda mfupi katika chama hicho.

Jamaa huyu anatabiriwa kuja kuwa mwanasiasa machachari kwa kuwa sio muhoga kabisa pale anapoamua kusema ukweli na vita yake kubwa ni kutaka uchumi umilikiwe na mtu mweusi.


Ushawishi alionao ndio umemfanya aangie katika orodha ya watu wenye ushawishi duniani kwa kuwa na kufuatwa na kusikilizwa na watu wengi.Hivi sasa baadhi ya vyama vikongwe vimeanza kumuhofia yeye na chama chake kutokana na nguvu aliyonayo hapa na kesho chama chake kinakwenda katika ilani ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu.
 
Picha mbalimbali zikimuonyesha Julius Malema akiwa huko Limpopo wakati akienda mahakamani hivi karibuni.


0 comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

About

 
Tricks and Tips