Blogger Tricks

LINKS

Saturday, 15 February 2014

ANGALIA PICHA.KAMA HUWAJUI POLISI WA AFRIKA KUSINI WAANGALIE HAPA WENYEWE NI DAKIKA MOJA MBELE

Nchi ya Afrika Kusini ni nchi ambayo huwezi ifananisha na nchi yoyote katika bara la Afrika kwa kuwa na polisi wengi kupita na unavyofikiria.
                         Polisi hao wakiwa tayari kwa kazi hapa Afrika Kusini

Kutokana na uhalifu uliokithiri katika nchi hii kuna idara tofauti za polisi zinazidi hata hamsini na kila idara ina kazi yake.Polisi wa nchi hii kama utafika kwa mara kwanza hapa Afrika Kusini unaweza ukafikiri upo katika nchi ya Marekani kwa kuwa kila kona unayopita utakuta

Friday, 14 February 2014

ANGALIA PICHA KILICHOTOKEA KATIKA MAANDAMANO YA CHAMA KIKUU CHA SIASA HAPA A.KUSINI CHA DA DHIDI YA ANC

 Chama siasa cha DA kinachoongozwa na bi.Helen Zille juzi kiliitisha maandamano makubwa ya wanachama wake hapa Afrika Kusini.Maandamano hayo yaliokuwa na lengo moja tu kufeli kwa chama cha ANC katika ahadi zake.,
                                  Magari ya polisi yakiimarisha usalama kabla

Tuesday, 4 February 2014

JE?,UNAJUA JIJI LA JOHANNESBURG LIMEPEWA HESHIMA NYINGINE YA KUANDAA MICHUANO MIKUBWA YA GOLF DUNIANI? NA HIKI NDICHO KINACHOENDELEA SASA HAIVI KATIKA VIWANJA HIVYO VYA GOLF HAPA JOHANNESBURG.ANGALIA PICHA UJIONEE KILICHOJIRI

Jiji la Johannesburg kwa mara nyingine limepata heshima ya kuandaa mashindano


ya golf kimataifa ya golf ambayo yameshirikisha washiriki toka nchi 24 dunianI.

Kwa hapa Afrika nchi zilizotuwakilisha katika mashindano hayo ni Afrika Kusini yenyewe,Zimbabwe na kwa upande wa Afrika Mashariki tumebahatika kuwakilishwa na nchi ya Kenya.

Jiji la Johannesburg limebahatika kufanikiwa andaa mashindano hayo baada ya kufuzu kwa vigezo vyote  vilivyotakiwa na wahusika.

Kabla ya mashindano hayo kuanza leo hii hapo jana katika Hotel ya HILTON iliyopo Sandton katika jiji hili la Johannesburg kuliandaliwa hafla maalumu na jiji la Johannesburg katika kile walichokiita kama ufunguzi wa mashindano

Monday, 3 February 2014

UMESHAWAHI LISIKIA JENGO REFU KABISA BARANI AFRIKA? JE,UNALIJUA WAPI LILIPO NA LINAITWAJE?UNGANA NAMI NKUPASHE KAMA HUJUI

Carton Centre ndio jengo refu kabisa kabisa barani Afrika mpaka sasa hivi kutokana na urefu wake hakuna jengo lolote lile lingine barano Afrika ambalo linalifikia jengo hili.

Jengo hili liko katika nchi ya Afrika Kusini katika jiji mama au jiji maarufu kabisa kwa kila kitu la Johannesburg au ukipenda liite city of gold.

Katika mitaa ya comissioner na small au comissiner von weiligh ndio utalikuta jengo mahali lilipo.Urefu wa jengo hili kwenda juu ni zaidi  ghorofa 52 ambazo uwezi kuta popote pale Afrka.Ndani ya jengo kuna kila kitu unachotaka na kabla ya kuwa ofisi za kawaida hapo nyuma zilikuwa ofisi za serikali kabla ya kuhamishiwa pritoria
Hilo jengo la katikati ndio Carton centre yenyewe ambayo ukiwa juu ya hilo ghorofa unaweza iona Johannesburg kwa ukubwa wake wote.

Sunday, 2 February 2014

KAMA UNAFIKIRI TATZO LA WAFANYAKAZI KUTOLIPWA MISHAHARA YAO LIKO TANZANIA TU BASI UNAJIDANGANYA ANGALIA PICHA HIZI HAPA AFRIKA KUSINI NA UJIONEE MWENYEWE

Wafanyakazi wa idara ya afya toka sehemu mbalimbali hapa Afrika Kusini,haivi majuzi waliandamana kwa wingi kabisa kushinikiza kulipwa mishahara yao ambayo hawakupata toka mwaka jana mwezi mwezi wa 10

Baada ya kuona serikali ya hapa imekaa kimya na walishafanya juhudi zote kufuatilia pesa zao wafanyakazi hao wakaja na mbinu maarufu kabisa inayotumika hapa Afrika Kusini inayofahamika kama( TOI TOI) yani maandamano.

Wakiwa wamebeba mabango yaliondikwa kuitishia serikali kuwa bila malipo yao hakuna kupiga kura mwaka huu wafanyakazi hao walikwenda piga kambi katika eneo linaloitwa braamfontein wakimtaka waziri anayehusika aje waongee nae

Hao ndio wafanyakazi wa wanaotoa huduma ya afya katika jiji hili la johannesburg katika maandamano ya hapo juzi kushinikiza malipo yao,unaweza soma walichokiandika katika mabox yao hapo juu

ANGALIA PICHA HIZI KATIKA KIKAO CHA CHAMA CHA SIASA CHA AGANG SA KILICHOTOA MSIMAMO WAO KUMHUSU KIONGOZI WAO ALIYEKIMBILIA KATIKA CHAMA CHA DA DR MAMPHELE RAMPHELA

Baada ya kukihama cha alichokianzisha yeye mwenyewe na kukimbilia chama cha siasa cha DA dr Mamphele Ramphela ambaye ametengeneza head lines za kufa mtu hapa Afrika Kusini kwa wiki hii baada ya kukihama chama chake bila ya kuwaambia viongozi wake na wanachama anaowaongoza,kesho yake baada ya uamuzi wake huo viongozi wake nao wakaja na tamko la chama hicho.

Angalia picha mbalimbali hapo chini za viongozi hao na wanachama katika mkutano na waandishi wa habari tarehe 29 mwezi wa kwanza katika ofisi za cham hicho hapa Johannesburg ambapo walisema wao bado wanamtambua Dr Mamphele Ramphela kama bosi wao na wanamsubiria katika haje hawapangie mkakati wa uchaguzi mkuu ujao.Kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu hapa Afrika Kusini kuna mambo yatakayoushangaza ulumwengu huu tokea hapa.

BAADA YA TIMU YA SOKA YA AFRIKA KUSINI KUVURUNDA KATIKA MICHUANO YOTE WALIOINDAA,JE UNAUJUA MPANGO WALIOKUJA NAO MAKOCHA WA HAPA KULISAIDIA TAIFA HILO?

Makocha wa zamani pamoja na wachezaji wa wa timu ya taifa ya Afrika Kusini wamekuja na mpango kabambe unaoitwa okoa Afrika Kusini.Mpango huo unakuja baada ya timu ya taifa ya hapa kufanya vibaya katika michuano yake yote walioindalia kuanzia kombe la dunia la mwaka 2010,kombe la mataifa ya Afrika ya mwaka 2012,kombe la mataifa ya Afrka mwaka 2013 pamoja na kombe la mataifa ya Afrka kwa wachezaji wa ndani 2014.

Hali hyo ikaleta mtafaruku wa wapi timu ya taifa ya mpira wa miguu inakoelekea na hivyo kupelekea waziri wa michezo wa hapa mh.Fikile Mbalula kuwaita wachezaji hao katika kugha ya kigeni kuwa ni BUNCH OF LOOSERS.

Baada ya matokeo hayo yote mabaya ya timu kwa udhamini wa benk ya NEDBANK sasa imechukua makocha wa zamani kama lashe Mashaba aliyekuwa kocha wa vijana chini ya umri wa miaka 23.Owen Dagama aliyekuwa kocha wa platinum stars pamoja na mchezaji wa zamani wa timu hiyo na pia ni kocha msaidizi wa Kaiza Chief.Makocha hao sasa wameenda kila jimbo la hapa Afrka Kusini na kutafuta vipaji  ambavyo viatakuja kuwa mwakilishi wa taifa hili hapo baadae.Angalia picha hizo tofauti katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Ligi kuu ya Afrika Kusini na kuwatambulisha baadhi ya wachezaji hao hapo juzi.
 

Blogger news

Blogroll

About

 
Tricks and Tips