BUNGE
maalum la Katiba, Jana Alhamisi Machi 6, 2014, liligeuka uwanja wa
“Mapambano” kama ile vita iliyotikisa ulimwengu, vita ya Kosovo kule
eneo la Balkan.
Hata
hivyo sio mapambano ya ngumi bali Majibishano makali yalizuka wakati
wajumbe wakiendelea kujadili kanuni zitakazokuwa dira ya kuliongoza
bunge hilo maalum, ambalo linaketi pale “mjengoni” kwenye ukumbi wa
Bunge la Tanzania mjini Dodoma.
Mwenyekiti
wa muda wa Bunge hilo, Pandu Ameir Kificho, alilazimika kuliahirisha
bunge hilo kwa takriban masaa manne, baada ya sintofahamu iliyohanikiza
ukumbi huo unaochukua takriban watu 700.
Malumbano
hayo yalikuwa ni kati ya wajumbe na mwenyekiti wakati mwingine wajumbe
kwa wajumbe, picha kadhaa zilizopigwa na waandishi wa habari wakati
sakata hilo likiendelea, zinaonyesha, wajumbe kama vile, Christopher Ole
Sendeka, Waziri wa sheria na katiba wa Zanzibar, Abubakar Khamisi
Bakari,Moses Machali na wajumbe wengine kadhaa, wakitoa maneno makali
dhidi yao wao wenyewe na wakati mwingine wakimtuhumu mzee Kificho kwa
upendeleo.
Baadhi
ya wajumbe wa bunge hilo, kama Halima Mdee, kuna wakati alionekana
akiwa ameshikwa na butwaa asiamini kinachoendelea ukumbini.
Kasheshe
hizo zinajiri huku wajumbe hao wakiwa hata kuapishwa bado, na
wachambuzi wa mambo wanabashiri kuwa hata mpango wa Ikulu wa kutaka
hotuba ya uzinduzi wa bunge hilo kufanyika wiki hii huenda usifanikiwe
kwani hata uchaguzi wa mwenyekiti bado kufanyika na kazi ya kuapisha
wajumbe hao zaidi ya 600 huenda ikachukua hadi siku tatu.
|
0 comments:
Post a Comment