Cristiano Ronaldo akimruka kipa wa Levante, Keylor Navas
MWANASOKA
bora wa dunia, Cristiano Ronaldo ameipaisha kileleni mwa LIga timu ya
Real Madrid baada ya kufunga bao zuri la kichwa akiruka juu kama mcheza
mpira wa kikapu katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Levante usiku huu.
Ronaldo aliyefunga dakika ya 11
akiunganisha kona ya Angel Di Maria, pia alimsetia Marcelo kuifungia
Real Madrid bao la pili dakika ya 49 na akamponza David Navarro kutolewa
nje kwa kadi nyekundu.
Karabelas alifunga dakika ya 81
kuipa Real bao la tatu, hiyo ikiwa mechi ya 29 wanacheza bila kufungwa.
Real sasa inatimiza pointi 67 baada ya kucheza mechi 27 na kutulia
kileleni, ikifuatiwa na Atletico Madrid pointi 64 baada ya mechi 27,
wakati mabingwa watetezi, Barcelona ni ya tatu kwa pointi zake 63 baada
ya kucheza mechi 27 pia.
0 comments:
Post a Comment