lazima
uzungumze Kiingereza. Inafaa tuzungumze lugha yetu,” Rais Yahya
Jammeh alisema hayo wakati wa kuapishwa kwa Jaji Mkuumpya nchini
humo. Tangazo hilo lilitolewa miezi michache baada ya nchi hiyo
kutangaza inajiondoa kutoka Jumuiya ya Madola, inayojumuisha mataifa 54
yaliyokuwa chini ya ukoloni wa Uingereza. Gambia ilisema “haitakuwa
tena mwanachama wa taasisi ya ukoloni mamboleo”. Uingereza ilionya hivi
majuzi kuhusu pingamizi la rais huyo dhidiya Uingereza, ambaye mwaka
jana alishutumu Uingereza na Amerika kwa kuandaa majaribio ya mapinguzi
ya Serikali nchini humo.
Rais wa Gambia mwaka jana aliiambia dunia kupitia Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba tishio kubwa linalotishia
ustaarabu na utu wa mwanadamu ni kuwepo kwa kampeni na uhamasishaji wa Ushoga na usagaji. "Wale wote wanaokuza
ushoga ni kama wanataka kukomesha kuwepo kwa binadamu",aliuambia mkutano
wa viongozi wa Dunia mjini New York kwa mujibu wa Gazeti la Huffington
Post."Hili ni janga na sisi waislamu na waafrika tutapigana kumaliza
tabia hii".Aliongeza kwa kusema,"Ulawiti katika namna yoyote ile ni uovu
na ni kama kupambana na Mwenyezi Mungu. Hata kama italazimishwa
kwa nguvu fulani kuwa ni haki kwa mwanadamu". "Gambia ni nchi
ya waumini. Dhambi na matendo ya zinaa yapolakini Ushoga si
wa kuvumiliwa katika nchi ya Gambia", aliongeza Rais Yahya Jammeh. Awali
aliwaambia mashoga waondoke nchini Gambia au watakatwa vichwa.
Mahusiano ya jinsia moja nchini Gambia ni haramu.Mwaka 2009
Jammeh aliwaambia maafisa wa jeshi waliopandishwa vyeo
kwamba, hatutahamasisha usagaji na ushoga katika jeshi, Ni mwiko katika
majeshiyetu,"Ntamfukuza mwanajeshi yoyote atakaye tuhumiwa kuwa Shoga au
Msagaji katika Gambia. Sisi hatuna haja ya Mashoga katika majeshi
yetu", alisema Rais huyo.
Rais wa Gambia Yahya Jammeh
0 comments:
Post a Comment