KIJANA ATEKETEZWA KWA MOTO BAADA YA KUHISIWA KUWA NI MWIZI WILAYANI KAHAMA
Kijana
mmoja anayesadikiwa kuwa ni mwizi ambaye jina lake halikuweza
kufahamika mara moja amefariki dunia baada ya kuchomwa moto na Wananchi
wanaodaiwa kuwa na hasira, katika kijiji cha Kagongwa Wilayani Kahama
Mkoani Shinyanga.
Kwa
mujibu wa mashuhuda tukio hilo limetokea jana majira ya Saa saa mbili
usiku kufuatia marehemu kujaribu kukodisha Usafiri wa pikipiki maarufu
kama bodaboda kwa lengo la kwenda Kijiji jirani cha Mwankumba.
Imeelezwa
kuwa madereva hao wa bodaboda walishtuka kuoa mtu huyo akiwa amevaa
koti kubwa, ndipo walipomuliza ili kujua vitu alivyobeba, na ndipo
alipojaribu kukimbia kabla ya kukamatwa na wananchi waliokuwepo katika
eneo hilo.
Hata
hivyo baada ya Kijana huyo kukamatwa amekutwa akiwa na Mapanga mawili
aliyoyaficha ndani ya koti, jambo lililopelekea wananchi hao kuchukua
jukumu la kumchoma moto wakimuhisi kujihusisha na matukio ya wizi.
Baada
ya tukio hilo Jeshi la Wilayani Kahama limefika eneo hilo na kuchukua
mwili wa marehemu ambao kwa sasa umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya
ya Kahama, huku uchungizi zaidi wa tukio hilo ukiendelea.
0 comments:
Post a Comment