Rais wa
Kenya Uhuru Kenyatta, ameamuru maafisa wakuu watendaji wa mashirika ya
serikali kukubali mishahara yao kukatwa kwa asilimia 20, la sivyo
waachishwe kazi.
Akiongea kwenye kongamano la kitaifa
kuhusu gharama kubwa ya matumizi ya
serikali, Rais Kenyatta alisema kuwa hatua yake na naibu wake pamoja na baraza la mawaziri kupunguza mishahara yao kwa asilimia 20 haikuwa kwa sababu ya kufurahisha watu.
serikali, Rais Kenyatta alisema kuwa hatua yake na naibu wake pamoja na baraza la mawaziri kupunguza mishahara yao kwa asilimia 20 haikuwa kwa sababu ya kufurahisha watu.
Kadhalika Kenyatta ameongeza kusema kuwa
uchumi wa nchi hauwezi kuwa mzuri ikiwa kila mtu anataka nyongeza ya
mishahara badala ya kuzingatia kupunguza gharama ya maisha na uzalishaji
wa bidhaa.
''Wakuu wa mashirika ya serikali
watatakiwa kukubali mishahara yao kupunguzwa kwa asilimia 20. Kuna
wakenya ambao wanaweza kushikilia nyadhifa hizo kwa pesa ndogo
ikilinganishwa na zile wanazopata wakuu hao,'' aliongeza kusema
Kenyatta.
Kenyatta amesema matumizi ya pesa za
serikali ni ya juu mno na kwamba hayawezi kudhibitiwa ikiwa baadhi ya
wafanyakazi wa sekta ya umma wataendelea kupata mishahara mikubwa.
Rais alisema lazima safari za kwenda nje
ambazo zinafanywa na baadhi ya wafanyakazi wa serikali, kupunguzwa.
Wakati huohuo, Rais aliwataka wabunge kukubali mishahara yao kukatwa
kwani ni baadhi ya wabunge anaopokea mishahara mikubwa duniani.
Swala la mishahara ya wabunge ni swala tete sana nchini Kenya.
Rais Kenyatta, alisema kuwa serikali
inatumia kati ya dola dilioni 4.6 kwa mishahara ya wafanyakazi wa umma
na kutumia dola bilioni 2.3 kwa maendeleo.
0 comments:
Post a Comment