Polisi wakidhibiti ulinzi katika barabara za Maiduguri
Mamia
ya wapiganaji wa kundi la Boko Haram, wamekabiliana vikali na wanajeshi
wa serikali huku milipuko na milio ya risasi ikisikika mjini Maiduguri
Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Wakazi wa mji huo wanasema kuwa walisikia milio ya risasi na milipuko kwa karibu saa mbili nyakati za Asubuhi.
Taarifa zinazohusiana
Siasa
Inaarifiwa
tukio hili limejiri wakati wa kile kinachoshukiwa kuwa shambulizi dhidi
ya kambi ya jeshi lililofanywa na wapiganaji wa Boko Haram.
Kuna
taarifa za mamia ya wapiganaji kuvamia mji huo asubuhi na mapema na
kushambulia kambi mbili rasmi za jeshi ili kuwaachilia wapiganaji
waliokamatwa na kuzuiliwa.
Wakazi walisema kuwa waliona ndege mbili za jeshi zikizunguka anga katika eneo hilo.
Jeshi linasema kuwa liliweza kutibua mashambulizi hayo na kusababisha majereha makubwa kwa washambuliaji hao.
Wakazi walioshuhudia makabiliano hayo walisema kuwa pande zote mbili zilipata majeraha.
Pia kumekuwa na taarifa ya milipuko kusikika ndani ya nyumba za wakazi pamoja na katika chuo kikuu cha Maiduguri.
Afisaa
mkuu wa haki za binadamu katika umoja wa Mataifa Navi Pillay -- ambaye
yuko nchini humo, alisema kuwa ukatili unaotendwa na wanajeshi ni sababu
ya kundi la Boko Haram kuendeleza mashambulizi.
Maelfu ya watu wameuawa nchini Nigeria katika kipindi cha miaka mitano tangu kundi la Boko Haram lilipoanza vita.
Ghasia hizi zimekithiri katika miezi michache iliyopita, licha ya juhudi za maafisa wa usalama kudhibiti usalama.
0 comments:
Post a Comment