Saturday, 8 March 2014
PICTURE OF THE WEEK-SMALL BOY ON TOP OF THE WORLD
Hii ndio ambayo leo hii nimeichagua kuwa ndio picha bora kabisa ya wiki.Ilikuwa ni katika mchezo wa kirafiki kati ya Brazil na Afrika Kusini uliofanyika siku ya jumatano ambapo timu hiyo ya Brazil iliifunga timu ya Afrika Kusini magoli 5-0.
Juu ya kilele kabisa ni mtoto ambaye alichepuka kuingia uwanjani na kujiunga na wachezaji wa Brazil kushangalia ushindi huo tukio ambalo kama limeweka historia vile kunakotokana na kuzoea kuona kila siku watu wazima ndio wanaingia uwanjani.
Mtoto huyo anayefahamika kwa jina la Ayo dosumun anaonekana akiwa juu kabisa ya wachezaji wa timu ya dunia ambayo ni Brazil wakishangalia pamoja ushindi huo,nyuma yake aliyevaa jaket jekundu ni baba yake Shola Dosumun akikimbia uwanjani hapo kumfuata mwanawe.
Unaionaje picha hii kama ungekuwa ni wewe au mwanao ndio huyo hapo juu?
Labels:
SPORTS
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment