Uongozi wa klabu bingwa ya Tanzania bara Dar Young Africans
umeonyesha mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine wa soka nchini siku moja
baada ya kurudi kutoka Misri walipoenda na timu kwenye mchezo dhidi ya
Al Ahly.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya klabu
hiyo ni kwamba viongozi wa msafara wa Yanga chini ya mkuu wa msafara
huyo makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga umerudisha kiasi cha
millioni 39 klabuni kutoka kwenye fedha walizopewa kwa ajili ya matumizi
kwenye safari yao nchini Misri.
"Eeh bwana safari hii kweli tuna viongozi wenye nia ya dhati ya
kuiongoza vizuri Yanga, Sanga na viongozi wenzie walioenda Misri
walipewa fungu la bajeti kwa ajili ya matumizi yote ya klabu nchini
Misri, lile fungu lilikuwa litumike lote, lakini tofauti na viongozi
wote wa misafara waliopita, Sanga na wenzake wameweza kurudisha millioni
39 kutoka katika fedha walizopewa. Haijawahi kutokea kwenye klabu hii
kwa kweli, huko nyuma kitendo kama hichi hakikuwahi kutokea, hapa
klabuni kila aliyesikia kuhusu hilo jambo ameshutushwa.
"Zile fedha zilikuwa tayari zimeshatolewa kwa matumizi hivyo hata
kama wangeamua kuzila hakuna ambaye angeulizia, hawa jamaa ni waadilifu
na wana mapenzi ya kweli na klabu," kilisema chanzo hicho cha habari.
0 comments:
Post a Comment