Picha zilizonaswa na mtambo wa satellite
Serikali
ya Uchina imechapisha picha zilizonaswa na mtambo wake wa satelite
zikionyesha mabaki ya kitu kipana kikielea katika bahari ya Kusini mwa
Uchina.Picha hizo zilipigwa siku ya Jumapili, saa ishirini na nne baada
ya ndege ya abiria ya Malaysia kutoweka ikiwa na abiria 239, lakini
haijabainika ikiwa vifaa hivyo ni vya ndege hiyo.Huku ikiwa na raia wake
154, ambao walikuwa abiria kwenye ndege hiyo ya Malaysia, serikali ya
Uchina imetuma mitambo kumi ya satellite kusaidia katika harakati za
kutafuta ndege hiyo.Picha za vifaa hivyo vitatu, ambavyo moja ina upana
wa takriban mita 24 kwa 22, zilichukuliwa siku ya Jumapili, siku moja tu
baada ya ndege hiyo kupotea, lakini zilichapishwa siku ya Jumatano.
Ubawa wa ndege hiyo iliyopotea ina upana wa mita sitini na moja.
Picha
hizo za satellite zimeweka vifaa hivyo takriban maili mia moja kutoka
kwa njia iliyotarajiwa kutumiwa na ndege hiyo na sio mbali kutoka kwa
kisima kimoja cha mafuta, ambako mfanyakazi mmoja aliripoti kuona kitu
kilichokuwa kikichomeka angani siku ya Jumamosi asubuhi.
Lakini siku chache zilizopita, kumekuwa na fununu kadhaa kuhusiana hatma ya ndege hiyo lakini zote zimekuwa uongo.
Makundi
ya uokozi hiyo vile vile wanatafuta mabaki ya ndege hiyo katika maji
inayokaribiana na rasi ya Malaysia, kwa sababu wanaamini kuwa ndege hiyo
ya Malaysia ilibadili mkondo na kuelekea Magharibi.
0 comments:
Post a Comment