Kocha wa Manchester United David Moyes ameandika barua ya wazi kwa
mashabiki wa klabu hiyo akielezea kwamba msimu wake wa kwanza ndani ya
klabu umekuwa m'bovu zaidi kuliko ilivyotegemewa.
Akiwasifu mashabiki kwa uvumilivu wao, Mscotish ambaye aliteuliwa na
Sir Alex Ferguson, amekiri kwamba matokeo yao mabovu yamemshangaza mpaka
yeye lakini ana uhakika kila kitu kitakaa sawa mbeleni.
"Wakati nilifahamu hii kazi ingekuwa na changamoto nyingi wakati
nilipopewa jukumu hili, lakini msimu mgumu tulionao hakikuwa kitu
ambacho nilikifiria, jambo ambalo nina uhakika mashabiki wote
hawakudhani hali ingekuwa hivi," aliandika Moyes.
"Wachezaji wangu, na makocha wenzangu wanajaribu kwa kila kuhakikisha timu inarudi katika kufanya vizuri.
"Wote tumezoea kuiona Manchester United inayofanikiwa na sapoti
mliyowapa wachezaji na mimi katika kipindi chote cha msimu ni kubwa
sana. Tunapocheza ugenini mashabiki wetu waliosafiri wameendelea kuwa
bora kabisa katika nchi hii na wakati tunapokuwa Old Trafford imani yenu
kwenye timu imekuwa ikionekana wazi.
"Kuisapoti timu yenu wakati inashinda ni rahisi lakini ni ngumu sana
wakati mambo yanapokuwa yanaenda vibaya, nyinyi mmekuwa nasi katika
kipindi chote."
"Kila magumu tunayopitia yatatufanya tuwe bora zaidi, timu imara na klabu bora huko mbeleni.
"Kwa miaka mingi sasa mmekuwa mkishuhudia vikosi vya ushindi na kwa
muda fulani, nina uhakika kabisa tutaiona Manchester United tuliizoea."
0 comments:
Post a Comment