Blogger Tricks

LINKS

Friday, 7 March 2014

ANGALIA PICHA-MJAMZITO ALIPOAMUA KULITOSA GARI LAKE BAHARINI HUKU KUKIWA NA WATOTO NDANI


Mama alivyopeleka hili gari mpaka baharini kwa makusudi

Screen Shot 2014-03-07 at 5.21.35 AM
Hii imetokea Marekani ambapo mama huyu mwenye umri wa miaka 32 akiwa ni mjamzito, aliamua kuliendesha gari hili na kuliingiza kwenye bahari kwa makusudi huku watoto wake wakipiga kelele kwamba mama anajaribu kutuua.Watoto wa Mwanamke huyu ambae imeripotiwa kwamba bado yuko hospitali akifanyiwa vipimo vya matatizo ya akili, ambao wana umri wa miaka
mitatu, tisa na 10 walichukuliwa na Idara ya watoto na familia kwenye jimbo la Florida baada ya kupata matibabu.Watoto hawa wote walikuwemo kwenye gari hili lililolengeshwa baharini na mama yao ambae anadai alikua anakwenda kwenye sehemu salama ambayo mume wake walieachana asingeweza kuwafata au kujua waliko.

Screen Shot 2014-03-07 at 5.23.08 AM
Wakati hili tukio linatokea alikuepo karibu Mtalii raia wa Canada ndio maana video ya tukio na hizi picha zimepatikana zikionyesha kila kitu.

Huyu ni miongoni mwa watu waliojitokeza kuokoa baada ya kusikia kelele za mtoto aliekua ndani ya gari akisema 'mama yetu anatuua'
Huyu ni miongoni mwa watu waliojitokeza kuokoa baada ya kusikia kelele za mtoto aliekua ndani ya gari akisema ‘mama yetu anatuua’

0 comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

About

 
Tricks and Tips