...Askari
maji wa singapore wakiendelea kutafuta ndege hiyo wakiwa umbali wa
kilometa 700 kazikazini mwa Singapore na kusini mwa china.
Maafisa wa
Serikali ya Malaysia waliokuwa wanadadisi picha zilizopigwa na mtambo wa
Satelite wa China ikionyesha kinachodhaniwa kuwa mabaki ya ndege
iliyotoweka, Jumamosi, wamesema kuwa mabaki hayo yalitoweka na huenda
sio mabaki ya ndege hiyo iliyotoweka siku ya jumamosi.
Waziri wa Ulinzi wa Malaysia Hishammuddin Hussein, pia amekanusha madai ya Marekani kwamba ndege hiyo ilipaa kwa masaa mengi kabla ya kutoweka na kupoteza mawasiliano
Waziri wa Ulinzi wa Malaysia Hishammuddin Hussein, pia amekanusha madai ya Marekani kwamba ndege hiyo ilipaa kwa masaa mengi kabla ya kutoweka na kupoteza mawasiliano
Amewaambia
waandishi wa habari mjini Kuala Lumpar kuwa picha hizo zilizopigwa siku
ya Jumapili,saa ishirini na nne baada ya ndege ya abiria ya Malaysia
kutoweka na abiria 239 zinadaiwa zilitolewa kimakosa na maafisa wa
China.
Aidha tetesi kuwa kifaa cha kupeperusha matangazo cha ndege hiyo kimekuwa kikituma taarifa imesemekana kuwa si ukweli .
Waziri huyo amesema kuwa kupotea kwa ndege hiyo sio kitu kilichotararajiwa.
Picha hizo zilitolewa na idara ya serikali ya China ya sayansi na teknolojia siku ya Jumatano.
Bwana Hussein kadhalika amekanusha ripoti ya jarida la Wall Street kwambandege hiyo ilituma data ya Engine yake kwa karibu saa 4 kabla ya kupoteza mawasiliano na kituo cha trafiki ya ndege.
Amesema kuwa juhudi za kuisaka ndege ghiyo zingali zinaendelea.

0 comments:
Post a Comment